Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Mbelgiji atua Simba

10755 Kocha+pic.png TanzaniaWeb

Thu, 5 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wamemleta kimyakimya Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mfaransa Pierre Lechantre.

Kocha Aussems aliyewahi kuzinoa timu kadhaa zikiwamo za Ligi Kuu ya Ufaransa, ES Toyes AC na Stade de Reims pamoja na mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2012, AC Leopards ya Congo yupo nchini tangu Jumapili.

Mbelgiji huyo mwenye miaka 53 na aliyecheza kama beki enzi zake za uchezaji akiwa na urefu wa futi 6 na inchi 3, aliishuhudia Simba ikiinyuka APR ya Rwanda kwa mabao 2-1 na jana pia alishuhudia tena Simba ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Singida United. Mechi zote hizo ni za Kombe la Kagame.

Mwananchi limedokezwa kuwa, Kocha huyo yupo katika mazungumzo ya mwisho ya mabosi wa Simba kabla ya kupewa kazi ya kuinoa timu hiyo itakayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika zitakazoanza Desemba mwaka huu.

Inaelezwa Mbelgiji huyo aliyezichezea klabu za RCS Vise, Standard Liege, KAA Gent, RFC Seraing zote za kwao Ubelgiji na ES Troyes AC anaendelea kufanya mazungumzo na mabosi wa Simba na kama watakubaliana ataanza kuifundisha kwa msimu ujao.

PATRICK NI NANI?

Patrick Winand Aussems alizaliwa, Februari 6, 1965 na sifa yake kubwa ni kuiwezesha AC LĂ©opards kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Congo Brazzaville mwaka 2014 bila kupoteza hata mchezo mmoja na ikifungwa bao moja tu.

Pia aliiwezesha timu hiyo katika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho ikipoteza mbele ya Sewe Sports ya Ivory Coast, hiyo ikiwa ni baada ya kung’olewa Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huo.

Alipotoka AC Leopard alichukuliwa El Hilal ya Sudan kabla ya kutemwa miezi michache baada ya timu kupata matokeo mabaya na kutua timu ya taifa ya Nepal aliyoinoa kati ya 2015-16.

Chanzo: mwananchi.co.tz