KAIMU kocha mkuu wa Simba, Masoud Djuma, amezidi kuwajaribu wachezaji wake katika kila mchezo kwenye Mashijdano ya Kagame yanayoendelea nchini.
Katika mchezo dhidi ya APR aliwapa nafasi Meddie Kagere na Adam Salamba katika upande wa ushambuliaji lakini katika mchezo dhidi ya Singida United uliopigwa leo, amewapa nafasi Kagere na Moses Kitandu.
Katika upande wa kipa kwenye mchezo uliopita alimuanzisha Ally Salim lakini katika mechi dhidi ya Singida alimuanzisha kipa mpya Deogratius Munish 'Dida'.
Katika mchezo uliopigwa leo katika Uwanja wa Taifa, Simba walionekana kutawala mpira lakini mbinu zao zilikuwa ngumu kupita kwa Singida United.
Singida walionekana kucheza kwa mipango zaidi kwa kucheza mpira wa kutulia, huku katika safu ya ushambuliaji iliyokuwa ikiongozwa na Habib Kyombo na Danny Lyanga.
ktika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Medie Kagere lakini Singida wakachomoa kupitia kwa Dany Lyanga aliyeunganisha mpira uliogonga mwamba baada ya Habib Kyombo kuupiga.
Kwa matokeo haya Simba na Singjda wote kwa pamoja wamefikisha pointi 7.