Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha KVZ: Zanzibar haiwezi kufanya vizuri bila wachezaji wa kulipwa

Fdfb551df78344b40dac932521525c8e Kocha KVZ: Zanzibar haiwezi kufanya vizuri bila wachezaji wa kulipwa

Mon, 7 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa timu ya KVZ Sheha Khamis amesema ili Zanzibar iweze kusonga mbele kwenye michuano ya kimataifa ni lazima timu zake ziwe na wachezaji wa kulipwa kama ilivyokuwa zamani.

Khamis alitoa kauli hiyo baada ya kumalizika kwa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Amal Atbara ya Sudan na kuondolewa kwa jumla ya mabao 4-0.

Alisema wakati wakicheza mpira klabu zilikuwa na mchanganyiko wa wachezaji wa ndani ya Tanzania na wengine kutoka nje na kufanya klabu hizo kuwa na ushindani.

“Tofauti na sasa timu inashiriki Ligi ya Mabingwa au Kombe la Shirikisho lakini inajengwa na wachezaji wa Zanzibar pekee, huwezi kushindana kabisa,” alisema.

Aliongeza “Katika mashindano lazima upate wachezaji wa kimataifa enzi zetu tulikuwa nao lakini uchumi ndio unakwaza, kama tunataka tufanikiwe lazima iwe hivyo, Zanzibar tushawahi kufika mpaka nusu fainali kwenye mashindano haya lakini timu zilikuwa nzuri na zilikuwa na wachezaji wa kimataifa,”.

Hata hivyo alisema kufungwa mchezo huo wa marudiano kulichangiwa na viungo wa kati ambao walicheza chini ya kiwango tofauti na walipocheza ugenini.

“Viungo hasa wa kati walituangusha sana na hata yale mabao ambayo tumefungwa yalikuwa ni mabao rahisi sana,” alisema.

Alisema matokeo yaliyojitokeza yamepangwa ingwa wao walijipanga kwa ajili kushinda na lililotokea ni mipango yake Mungu.

“Hili limepangwa na Mungu tulijipanga kushinda lakini haikuwa rahisi niseme tu hapa nidhamu ya mchezo ilipotea nyumbani kuliko ugenini,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz