Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Biashara United aanza kuonja shubiri

18419 Pic+biashara TanzaniaWeb

Fri, 21 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa Biashara United ya Mara, Mrundi Hitimana Thiery amesema ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara imekuwa kikwazo katika mashindano hayo.

Akizungumza jana, Thiery alisema ratiba hiyo inachosha wachezaji na kuzipa wakati mgumu timu kushindana kikamilifu kwa kuwa mechi zinachezwa ndani ya muda mfupi.

Biashara United jana jioni iliikaribisha Azam katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume mkoani Mara.

Timu hiyo iliyopanda daraja, imecheza michezo minne imeshinda moja, imetoka sare moja, imepoteza miwili na ina pointi nne ikiwa nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi.

“Ratiba imekuwa sio rafiki kwetu mechi zinakaribiana unacheza leo baada ya siku mbili mechi nyingine, hakuna muda mzuri wa maandalizi na kusahihisha makosa.

“Wanaopanga ratiba wanapaswa kuangalia jambo hili, ukiangalia ligi haina mdhamini timu zinatakiwa kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa muda mfupi, “alisema Thiery.

Pia Thiery alisema Biashara imeshindwa kupata matokeo mazuri kwa madai kuwa timu hiyo inaundwa na idadi kubwa ya wachezaji chipukizi.

Kocha huyo alisema anatarajia timu hiyo itafanya vyema katika mechi zinazofuata ingawa ameahidi kuchukua hatua kwa kuongeza kasi kwenye mechi zinazofuata.

Chanzo: mwananchi.co.tz