Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp aanza visingizio akijiandaa kuivaa Atletico

Dfed1a65fbc13d67301ed47a3dbaf975 Klopp aanza visingizio akijiandaa kuivaa Atletico

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema anamuheshimu Diego Simeone kocha wa Atletico Madrid, lakini havutiwi na staili ya uchezaji inayofundishwa na kocha huyo.

Liverpool itasafiri takribani kilomita 1446 kuwafuata Atletico katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya, utakaochezwa Uwanja wa Wanda Metropolitano saa 4:00 usiku.

Kuelekea mchezo huo, Klopp amesema hapendezeshwi sana na mtindo wa uchezaji wa timu hiyo wa, kuzuia wakati wote “hakuna atakayependa aina hii, hiyo ni kwa mimi, makocha wengine wanapenda mitindo tofauti, wanachoangalia wao ni matokeo tu, hivyo ndivyo Atletico walivyo,”amesema Klopp.

Katika kundi B, Liverpool inaongoza ikiwa na pointi sita, baada ya kushinda michezo miwili dhidi ya Milan na FC Porto, wabishi wa jiji la Atletico wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi nne, AC Milan wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi moja, FC Porto hawana kitu.

Msimu uliopita Liverpool walifungwa mabao 3-2 katika Uwanja wao wa Anfield na kufungwa tena bao 1-0 katika Uwanja wa Wanda Metropolitano na kuondolewa katika hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

Chanzo: www.habarileo.co.tz