Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiwango Simba CAF chatinga bungeni

Bunge2021 Ed Kiwango Simba CAF chatinga bungeni

Tue, 25 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Simba ambayo ilitinga hatua ya robo fainali baada ya kuongoza Kundi A, lililokuwa na bingwa mtetezi, Al Ahly ya Misri, timu kongwe ya DR Congo, AS Vita na wakongwe Al-Merrikh ya Sudan, Jumamosi iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, lakini ikatolewa kwa jumla ya mabao 4-3, kutokana na mchezo wa kwanza ugenini kufungwa 4-0.

Akizungumza bungeni jana, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema katika Uwanja wa Mkapa Jumamosi yalifanyika mambo makubwa.

“Kama Bunge lazima tupongeze kwa timu yetu ya Simba Sports Club kututoa kimasomaso kuweza kufika robo fainali ya Kombe la Mabingwa wa mpira wa miguu Afrika nzima, si padogo si haba,” alisema.

Aliongeza: “Kwa hiyo na wale rafiki zetu wengine nao wajitahidi badala ya ligi ya hapahapa tu, wajitahidi kidogo waige wasiogope, tunawategemea mwakani, hata Namungo wamejitahidi ni mara ya kwanza wameingia kwenye mashindano makubwa wamejitahidi. Sasa wengine mpo wapi? Badala yake tunakuwa tunashangilia wageni tu jamani hiyo haipendezi hata kidogo, lakini mwisho wa haya si tarehe 3 Julai (mechi ya Simba na Yanga) jamani ndio majibu yatapatikana baada ya hapo tutakutana kwenye ukumbi huu tusikie mambo yakoje,” alisema.

Chanzo: ippmedia.com