Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Yanga afungiwa

24891 Pic+banka.png TanzaniaWeb

Thu, 1 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kamati ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Zisizoruhusiwa Michezoni ya Kanda ya Tano Afrika ( RADO ) imetoa hukumu ya kumfungia mchezaji wa Yanga, Mohamed Issa 'Banka' kutokana na matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alisema Banka amefungiwa miezi 14 kwa kukutwa na hatia hiyo.

Anasema Banka amekuwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu aina ya bangi akiwa nchini Kenya.

"Banka alikutwa na hatia hiyo akiwa pale Machakos Kenya katika mashindano ya CECAFA Challenge Cup na kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar, " alisema.

"Hukumu yake hiyo itaanzia Desemba 9, 2017 ambapo alichukuliwa kwenda kufanyiwa vipimo na itamalizika Februari 2, 2019.

"Banka baada ya kupimwa alikubali kweli alitumia kwa kupitia kwa maandishi yaani barua na baada ya kukutwa na hatia ilitakiwa kufungwa maisha lakini baada ya kukubali alipunguziwa.

"Banka atakiwi kufanya mazoezi ya mbeli ya watu lakini kama atatumikia vizuri adhabu hiyo miezi miwili ya mwisho ataruhusiwa kufanya mazoezi na timu yake, " alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz