Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Kitaeleweka Nigeria"- Yanga

Yanga Kitaeleweka Kiungo wa Yanga, Feisal Salum akijaribu kumtoka mchezaji wa Rivers

Fri, 17 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benchi la ufundi la Wanajangwani Young Africans, wana imani kubwa kuwa wanakwenda kupindua meza dhidi ya Rivers united wikiend hii na kusonga mbele.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza Yanga walipokea kichapo cha bao 1-0 na kufanya kazi kuwa kubwa kwa kuhitajika wapate ushindi mkubwa ili waweze kusonga hatua inayofuata.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa wanamatumaini makubwa ya kupata matokeo katika mchezo wa marudio utakaochezwa Nigeria.

"Uwezo tunao na nia tunayo, jambo moja tu ambalo tunakwenda kulifanya ni kumpiga mpinzani wetu na tutafanya jambo ambalo litaisimamisha Afrika na dunia ya michezo,".

Yanga inakwenda nchini Nigeria, huku ikiwakosa wachezaji wake watatu wa Kimataifa, kiungo Khalid Aucho, beki Djuma Shabani na Straika Fiston Mayele ambao bado Shirikisho la Soka Afrika CAF, halijawapa ruhusa ya kushiriki michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live