Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya anachapisha kitabu cha kumbukumbu ya maisha yake baadaye mwaka huu, akisema anatumai kitabu hicho kitaonyesha "jinsi gani ulimwengu unaweza kuwakaribisha wale waliozaliwa tofauti".
Semenya ni mwanamke mwenye jinsia tofauti na amezungumza kuhusu masaibu aliyokumbana nayo katika kazi yake - ikiwa ni pamoja na kulazimika kutumia dawa za kukandamiza homoni ya testosterone, na kujitolea kuonyesha uke wake kwa maafisa wa riadha alipokuwa na umri wa miaka 18 ili kuthibitisha kuwa yeye ni mwanamke.
The Race To Be Myself itachapishwa mnamo Oktoba na Merky Books, uchapishaji ulioanzishwa na rapper wa Uingereza-Ghana Stormzy.
Semenya anasema umma unaweza kumfahamu kwa mafanikio yake katika Olimpiki, lakini "bado kuna mengi ninayohitaji kuhusisha kuhusu nguvu, ujasiri, upendo, uthabiti na kuwa mkweli kwa jinsi ulivyo."