Mwanariadha wa Kenya, Abel Mutai alikuwa amebakiza mita chache kumaliza mbio huku akiwa anaongoza lakini alama za kumaliza zikawa zimemchanganya akasimama.
Mwanariadha wa Hispania, Ivan Fernández ambaye alikuwa nyuma yake akajua kilichokuwa kinamtatiza Mutai, akampigia kelele aendelee kukimbia.
Mutai hakuwa anafahamu Kihispaniola. Hakuelewa. Fernández akajua Mutai hakuelewa akaamua kumsukuma mbele ili Mutai amalize mshindi.
Baadaye Mwandishi akamuuliza Ivan; "Kwanini umefanya hivyo?"
Ivan akajibu; "Ndoto yangu ni kwamba siku moja tutakuwa katika jamii ambayo tunasukumana sisi wenyewe na wengine kwa ajili ya kushinda."
Mwandishi akasisitiza kwa kuuliza; "Kwa nini ulikubali Mkenya ashinde?" Ivan akajibu; "Sikusababisha ashinde, ilikuwa lazima ashinde. Hizo zilikuwa mbio zake."
Mwandishi akaendelea kuuliza; "Lakini ungeweza kushinda mbio Ivan..!" Ivan alimtazama na kujibu; "Lakini nini ingekuwa faida ya ushindi wangu? Heshima ya medali yangu ingestahili? Mama yangu angefikiria nini?"