Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipyegon Bett wa Kenya afungiwa

12386 Pic+bet TanzaniaWeb

Fri, 17 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nairobi, Kenya. Mwanariadha chipukizi wa Kenya, mshindi wa medali ya shaba katika mbio za ubingwa wa Dunia mwaka 2017 katika mita 800, Kipyegon Bett, amefungiwa kushiriki riadha.

Mwanariadha huyo amefungiwa kutokana na kushindwa kujitokeza kuchukuliwa vipimo kwa ajili ya kuchunguza iwapo anatumia dawa za kuongeza nguvu zilizopigwa marufuku michezoni.

Chipukizi huyo mwenye miaka 20, ambaye aliutikisa ulimwengu wa riadha kwa kushika nafasi ya tatu katika ubingwa wa Dunia 2017 jijini London, Uingereza, akiwa na miaka 19, atalazimika kusubiri uamuzi mwingine.

Uamuzi huo wa kufungiwa umetolewa na kamati maalumu ya mchezo huo iliyopewa mamlaka na Shirikisho la riadha la kimataifa (IAAF), inayozuia matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni (AIU).

AIU imewataja wanariadha 120 waliochunguzwa na kitengo hicho akiwemo bingwa wa marathon wa Kenya, Samuel Kalalei na Lucy Kabuu.

Chanzo: mwananchi.co.tz