Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipimo cha MRI kukibomoa kikosi Serengeti

39687 Mri+serengeti+pict Kipimo cha MRI kukibomoa kikosi Serengeti

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha.Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema  wamelazimika kuongeza wachezaji wapya kwenye kikosi cha Timu ya Soka ya Vijana (Serengeti Boys) wakihofia kipimo cha MRI.

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau alisema timu hiyo sasa itakuwa na wachezaji 50.

Alisema wamelazimika kuongeza wachezaji wengine wakihofia baadhi ya waliokuwepo mwanzo kutokidhi vigezo watakapokwenda kwenye kipimo cha MRI.

"Tumeamua kuchukua tahadhari mapema, ili kuwachuja wale ambao wataonekana kuzidi umri isije kutokea kipindi cha mashindano," alisema Kidau na kufafanua.

 

"Tumefanya hivyo kwa kuwa hawa vijana, miaka imesogea, hivyo tunapaswa kujiridhisha mapema

Alisema vijana hao 50 watapimwa kipimo cha MRI mapema kabla ya kile watakachokuja kufanyiwa na CAF.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz