Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipigo mfululizo cha Simba chatua Bungeni, Spika atoa neno

40035 Pic+simbaa Kipigo mfululizo cha Simba chatua Bungeni, Spika atoa neno

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kipigo walichokipata timu ya Simba nchini Misri, bado kimemuumiza na kuwaumiza Watanzania wengine.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Februari 4, 2019 bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo amewataka Watanzania kuwa wazalendo na timu zao zinapocheza nje ya nchi.

“Asubuhi nilikutana na (George) Mkuchika akawa anaonyesha mkono na kunyoosha vidole vitano, nikakutana na Mwigulu Nchemba naye akawa ananifanyia kama anaendesha bodaboda, nikamuuliza Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) hii maana yake nini, daa ni kipigo cha juzi kweli tulipigwa jamani,” amesema Ndugai huku kelele za kushangilia zikitolewa na wabunge mashabiki wa Yanga

Wakati wote Mbunge huyo wa Kongwa akizungumza, kelele za kushangilia kwa wabunge kugonga meza zilitawala ambapo Ndugai amesema kipigo cha mfululizo kwa timu hiyo kwenye mashindano makubwa ya klabu bingwa kinawaumiza wapenzi na mashabiki.

Amewataka wapenzi wa timu nyingine kuunga mkono timu za wenzao wanapocheza na timu za nje ya nchi ili ukifika wakati wote wafanye vizuri.

Hata hivyo, aliwatania wabunge kuwa kilichoiponza Simba ni suala zima la baridi ambapo sasa timu ya Al Ahly ikija nchini watalazimika kucheza saa nane mchana ili nao wachezaji wao waumizwe na jua kali.



Chanzo: mwananchi.co.tz