Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipchonge hakamatiki mbio za wanaume Olimpiki

Kip Mwanariadha wa Kenya, Eliud Kipchonge

Sun, 8 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkimbiza upepo wa Kenya, Eliud Kipchoge kwa mara nyingine amedhihirisha ubora wake kama mfalme asiye na ubishi wa mbio za marathoni kwa kutwaa taji lake la Olimpiki kwenye mitaa ya Sapporo mapema leo.

Mshikilia rekodi huyo wa Dunia alitumia saa 2 dakika 08 sekunde 38 kushinda medali ya dhahabu, akiwa ni mtu wa tatu tu kushinda mbio za marathoni mfululizo.

Abdi Nageeye wa Uholanzi alishinda medali ya fedha kwa kutumia saa 2: 09.58, mbele ya Bashir Abdi wa Ubelgiji aliekamata nafasi ya tatu na kujinyakulia medali ya shaba.

Kipchonge mwenye umri wa miaka 36, huu ni ​​ushindi wake wa 13 katika marathoni 15 alizokimbia tangu mwaka 2013, na ushindi huu umekuja siku moja baada ya mwenzake Peres Jepchirchir kupata ushindi katika mbio za Olimpiki za wanawake.

Mbio hizo za Marathoni zilishuhudia wakimbiaji wapatao 106 wanaowakilisha nchi zipatazo 45.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live