Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa Mbambane kimewaka bwana

Tue, 4 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

KAMA Mbabane itang’olewa leo basi mtu aliyekuwa katika ramani ya kutemwa ni kipa wao namba moja, Sandanelwe Mathabela.

Taarifa zilizopo hapa ni kwamba, Mathabela mara baada ya kufika Manzini alilazimika kuomba radhi kwa bao ‘alilomzawadia’ mshambuliaji Meddie Kagere.

Meneja wa Uwanja, ambao utatumika kwa mchezo huo, Mangaliso Mkhantjwa alisema kwa Mathabela kufungwa mabao ya namna ile sio kitu cha kigeni kabisa.

Mkhantjwa alisema Mathabela alilazimika kuomba radhi, lakini bao hilo ndiyo linalowapandisha mlima Mbabane kuelekea mechi ya leo.

Mkhantjwa alisema mashabiki wa Mbabane wanaona kama timu ingekuwa na kazi nyepesi kushinda nyumbani 2-0 nyumbani, lakini kushinda 3-0 ni kazi nzito.

Hata hivyo, alisema Mbabane wanaweza kupindua matokeo kama hayo, walifanya hivyo mwaka 2016 waliposhinda nyumbani 3-0 baada ya kufungwa 4-1 na AFC Leopard ya DR Congo.

“Mathabela amekuwa katika wakati mgumu baada ya kupoteza mechi ya kwanza, anaaminiwa kwa uzoefu wake lakini anafungwa mabao ya kizembe mara kwa mara,” alisema Mkhantjwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz