Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa Bora ligi ya Mali kutua Yanga

DJUNG Kipa,Diarra Djigui

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Wananchi Yanga SC, wiki hii itamshusha kipa bora wa ligi ya Mali, Diarra Djigui anayekuja kuwa kipa namba moja wa timu hiyo ya Jangwani katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na mashindano ya kimataifa.

Djigui ambaye anatua Yanga akitokea klabu ya Stade Malien ambao ni mabingwa wa Mali, atasaini mkataba wa miaka miwili na Yanga.

Kipa huyo, mwenye miaka 26, ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Mali iliyoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanaocheza kwenye ardhi ya nyumbani (CHAN) 2020, ni chaguo namba moja la kocha wa Yanga, Mtunisia Nesreddine Nabi ambaye amekuwa akitafuta kipa anayemtaka.

Shoo nzima ya kuinasa saini Djigui imesimamiwa na bilionea wao Ghalib Mohamed ambaye ilibidi apande dau ili kumbadili mawazo kipa huyo ambaye alikuwa mbioni kutua katika klabu moja ya Afrika Kusini.

Djigui, ambaye alicheza fainali za Kombe la Dunia la Vijana U-20 (2015) na kuiwezesha Mali kumaliza ya tatu nyuma ya Serbia na Brazil, alikuwa mmoja wa makipa watatu bora katika fainali za CHAN 2020 zilizofanyika nchini Cameroon baada ya kuonyesha kiwango kikubwa hasa kuzuia michomo mikali wakifika fainali na kumaliza wa pili nyuma ya Morocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live