Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kindoki afichua ramani ya ubingwa Yanga

50040 KINDOKI+PIC

Wed, 3 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIPA namba moja wa Yanga sasa, Klaus Kindoki, amesema amebakiza hatua chache kurudi katika ubora wake anaoufahamu kabla ya kutua Tanzania na muda si mrefu atawashangaza waliokuwa wanamshambulia, lakini pia akataja njia sahihi waliyokubaliana ili Yanga ibebe taji msimu huu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kindoki alisema anakaribia kurejea katika kiwango chake na kuisaidia timu yake kufuzu kwa hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Alliance Jumamosi, wala sio jambo la kulijadili sana.

Kindoki alisema kuhusu mashabiki waliokuwa wanamzomea hazitapita mechi tano atawajibu kwa vitendo kwa kuwaonyesha uwezo wake halisi na akasisitiza hana mpango wa kuondoka klabuni hapo.

“Nakaribia kurudi katika ubora wangu wa awali, najijua nilikuwa wapi. Nakubali nilipofika hapa nilitaka kupotea kidogo, lakini sasa niko sawa na nimebakiza hatua chache kurudi kwenye ule uwezo wangu wa mwanzo.

“Ngoja zipite kama mechi tano kutoka hii ya juzi halafu wataona Kindoki halisi yukoje, nitawajibu kwa vitendo waliokuwa wananishambulia kuwa mimi ni kipa mbovu. Na natarajia kuwapo sana hapa Yanga, sitaondoka subirini,” alisema.

Kipa huyo alisema msimu huu kama siyo kubeba mataji yote mawili, basi watatwaa taji moja kati ya mawili wanayoyania sasa.

“Wachezaji tumekubaliana kufanya kitu tofauti kwa kuchukua mataji yote mawili. Lakini kama tutakosa moja, basi moja tulichukue na hilo linawezekana kabisa hakuna ugumu.”

Alisema wanaweza kupotea katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, lakini Kombe la FA wamekubaliana sio la kupishana nalo na katika mechi mbili zilizosalia wameziwekea mkakati mzito.

“Kwenye ligi tutaendelea kushindana. Wapinzani wetu wakifanya makosa itakuwa faida kwetu. Tunaweza kupoteza taji moja la Ligi Kuu lakini siyo hili la FA. Tumebakiza mechi mbili ambazo kila moja tumeipangia mkakati wake.”

Kindoki aliwatumia salamu wapinzani wao katika hatua ya nusu fainali, Lipuli FC ya Iringa akisema katika mchezo huo itakuwa ni zamu yao kuonja machungu ya kipigo.

“Wale Lipuli si walitufunga katika ligi? Tutarudi palepale. Mashabiki wa Yanga wasafiri kwa wingi waone kitakachotokea. Niliumia sana lile bao walilofunga. Katika mechi ijayo itakuwa zamu yao kulia, ” alisema Kindoki ambaye hakuwa na msimu mzuri alipoanza kuitumikia Yanga.

Kindoki afichua ramani ya ubingwa Yanga

Tuesday April 2 2019

By KHATIMU NAHEKA

Chanzo: mwananchi.co.tz