Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinda Serengeti Boys atuliza mzuka

50235 Pic+serengeti

Thu, 4 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Oscar Mirambo amewaondoa hofu Watanzania kuhusu afya ya mshambuliaji nyota wa kikosi hicho Kelvin John.

Kelvin aliibua hofu baada ya kuumia katika mchezo wa juzi jioni walioshinda mabao 2-1 dhidi ya Cameroon.

Mshambuliaji huyo alishindwa kuendelea na mchezo na kuibua hofu kwa mashabiki kama atakuwa fiti kucheza Fainali za Kombe la Mataifa Afrika zilizopangwa kuanza Aprili 14 hadi 28, mwaka huu.

Akizungumza kwa simu jana, Mirambo alisema kinda huyo yuko katika hali njema licha ya kupata jeraha la msuli.

“Kelvin alipata maumivu madogo na alipata matibabu akiwa chini ya uangalizi wa madaktari,”alisema Mirambo.

Akiizungumzia Cameroon, Mirambo alisema haukuwa mchezo mwepesi na amepongeza kazi nzuri ya wachezaji waliopambana kuipa matokeo mazuri timu ya Taifa.

Kocha huyo alisema ana matumaini mashindano hayo yatakuwa na tija kwa timu yake kwa kuwa imepata uzoefu wa kutosha baada ya kucheza na timu bora Afrika. Serengeti Boys kesho itacheza mechi yake ya mwisho na Rwanda.

Fainali za Afrika zitashirikisha nchi nane ambazo ni Tanzania, Nigeria, Angola, Cameroon, Guinea, Morocco, Uganda na Senegal.



Chanzo: mwananchi.co.tz