Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kina Msolla kumbe hawatanii

69541 Msolla+picha

Sat, 3 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema tayari wameshaanza kutimiza ahadi zao walizokuwa wanazitoa kwa wanachama kwa kuanza na suala la timu kuwa na jezi rasmi ambazo zitainufaisha klabu.

Alisema katika kampeni zake kitu kikubwa ambacho kilikuwa kinalalamikiwa na wanayanga ni uuzwaji holela wa jezi ambao ulikuwa hauinufaishi klabu.

Aliongeza hawana muda mrefu katika uongozi wao, lakini tayari wameshaanza kupunguza ahadi walizoahidi kwa kuzifanyia kazi na kuahidi kuwa huo ni mwanzo na wataendelea kufanyia kazi zaidi.

"Tangu tumeanza uongozi hata miezi mitatu haijakamilika, moja ya ajenda yetu namba nne ilikuwa ni kusimamia utawala bora na uadilifu."

"Kwa mara ya kwanza tumekuwa na jezi rasmi ambazo zitainufaisha klabu, ombi langu ni kuwaomba wanayanga kununu jezi rasmi," alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz