Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kina Dante mikononi mwa Zahera

68665 Pic+zahera

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Mshindo Msola amesema suala la wachezaji Andrew Vincent 'Dante', Kelvin Yondani na Juma Abdul anamuachia Kocha Mwinyi Zahera.

Hayo ameyasema Zanzibar leo alipokuwa akizungumza na wanachama wa klabu hiyo katika uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi visiwani Zanzibar.

Amesema anashangazwa na nyota hao kugomea kambi wakati ni wachezaji wote wa msimu ulioisha wanadai madai yao na tayali alikaa nao na kukubaliana waingie kambini wakati wao wakiendelea kushughulikia malimbikizo yao.

"Suala la wachezaji hao nimemuachia mwalimu ndiye atakayeamua kama kuna umuhimu wa kuwatafuta na kuwarudisha tutafanya hivyo na kama hakuna basi wataenfelea na mgomo wao," amesema Dk Msolla na kuongeza;

"Usajili uliofanywa msimu huu umezingatia kila idara hivyo mwalimu ambaye kawasiri nchini alfajili ya kuamkia jana na kuingia moja kwa moja kambini atatuambia kama wanahitajika."

Amesema kuna wachezaji wapo kambini Morogoro na wao wanamadai kama ya hao wachezaji na kuhoji hao wanauspesho gani ambao unawafanya washindwe kuwa waungwana kama wengine.

Pia Soma

Msolla amesema wao ndio kwanza wao ni wageni katika uongozi wa Yanga wanatakiwa kupewa muda ili kuyashughulikia malimbikizo ya madai waliyoyakuta.

"Madai yao yapo kimkataba na kisheria hakuna kiongozi hata mmoja aliyekataa kwamba anadaiwa na wachezaji hao hivyo ni jambo la kutumia busara," amesisitiza Dk Msolla aliyeiongia madarakani na viongozi wake Mei mwaka huu.

Chanzo: mwananchi.co.tz