Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilomoni aivimbia Simba

Thu, 1 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MWANACHAMA maarufu na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mwadhamini wa Simba,  Hamis Kilomoni amesema ataendelea kutekeleza majukumu yake kama mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa klabu hiyo, lichja ya kutangazwa kuenguliwa kwenye nafasi hiyo.

Hivi karibuni, Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Crescentius Magori na Wakala wa Usajili na Udhamini (Rita) walisema Kilomoni hatambuliwi kwenye nafasi hiyo tangu Novemba 2017.

Lakini mapema leo kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwake, eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, Kilomoni amedai hatambui uamuzi huo hadi atakapopewa barua rasmi kutoka Simba ya kutomtambua.

"Nilichaguliwa kuwa mdhamini kwa utaratibu maalumu na ninapaswa kuondolewa kwa utaratibu maalumu," alisisitiza Kilomoni.

Amesema bado anatambua nafasi yake hiyo ndani ya Simba huku akidai kwamba mwenye mamlaka ya kumuondoa ni uongozi wa Simba uliochaguliwa na wanachama tena kupitia Mkutano Mkuu wa Wanachama na sio kama ilivyofanyika sasa.

Chanzo: mwananchi.co.tz