Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilimanjaro International Marathon yafunga usajili

Kili Marathon.jpeg Kilimanjaro International Marathon yafunga usajili

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Zikiwa zimesalia wiki chache kabla ya kufanyika mbio ya Kilimanjaro International Marathon, wandaaji wa mbio hiyo wameeleza kufungwa kwa usajili wa washiriki msimu huu baada ya idadi iliyowekwa kufikiwa tangu wiki iliyopita

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waandaaji hao jana, usajili kwa ajili ya ushiriki wa mbio za Kilimanjaro Premium lager za kilomita 42 na ule wa kilomita 21 Tigo Half Marathon umefungwa rasmi.

"Hata hivyo bado usajili kwa ajili yam bio za kujifurahisha za Grand Malt 5km utaendelea, ila si kwa njia ya mtandao tena bali kupitia vituo vya kuchukulia namba Dar es Salaam (Februari 18 na 19), Arusha (Februari 21 na 22) na Moshi (Februari 23, 24 na 25)," imesema sehemu ya taarifa ya waandaaji.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa tarehe ya mwisho ya kujiandikisha kwa mbio hizo za kilomita 42 na kilomita 21 ilikuwa ni Februari 6, 2023 lakini kwa mujibu wa waandaaji, nafasi za kujiandikisha zilijaa kabla ya tarehe hiyo jambo lililopelekea zoezi la usajili huo uliofanyika kupitia tovuti yao.

"Tunawajibika kuchukua hatua hii ili kuakisi viwango vya kimataifa vilivyowekwa kuhusiana na usajili ili kuhakikisha maandalizi yanafanywa ili kuepuka changamoto ambazo si za lazima wakati wa tukio husika”, ilisema taarifa hiyo.

Iliongeza taarifa hiyo, "Hatua hii itatusaidia kama wandaaji wa mbio hizo kufanya maandalizi ya mapema, ikiwemo kuhakikisha uweko wa maji ya kutosha katika maeneo yatakayotumiwa na washiriki, medali za kutosha, vesti za kukimbilia pamoja na usalama wa uhakika kwa washiriki na eneo la Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ambako tukio litafanyikia".

Huku hayo yakijiri, waandaji wa mbio hizo pia wametoa onyo kali kwa wale wanaotajwa kuhusika na uuzaji wa tiketi kwa njia ya mtandao kinyume cha taratibu ambapo umeonya watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Kuna taarifa zinazodai ya kuwa kuna baadhi ya watu ambao si waaminifu wanauza tiketi za Kilimanjaro Marathon mtandaoni, tunatoa rai kwa wananchi kutoa taarifa kwa wandaaji iwapo watawabaini wanaofanya mchezo huo mchafu ili hatua zichukuliwe dhidi yao kwani usajili ushafungwa”, ilisema taarifa hiyo ya waandaji.

Waandaaji pia walionya dhidi ya washiriki wanaokimbia kwa kutumia namba za ushiriki zisizo za kwao kwa mujibu wa usajili ambapo uongozi huo umesema hautawajibika na changamoto yoyote itakayotokana na hali hiyo, ambapo pia umesema kuwa, watakaobainika kufanya hivyo hawatapokea medali na majina yao hayatawekwa kwenye orohda ya walioshiriki mbio hizo mwaka huu.

"Pia tumekuwa na visa vya watu kukimbia na kwa kutumia nambari za zamani, hawa nao wakibainika watachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwafungiwa kabisa kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathon,” iliendelea kusema taarifa hiyo ya waandaaji.

Chanzo: Mwanaspoti