Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichomtoa kifungoni Mwakalebela hiki hapa

Yanga Pic Mwakalebela Data.png Kilichomtoa kifungoni Mwakalebela hiki hapa

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemfungulia makamu mwenyekiti wa Yamga, Frederick Mwakalebela aliyekuwa amefungiwa kwa miaka mitano kujihusisha na soka na kulipa faini ya Sh7 milioni.

Mwakalebela alikumbwa na adhabu hiyo Aprili 2, akituhumiwa kwa kauli zake za kuishutumu TFF kutoitendea haki klabu yao hasa katika suala la kesi yao na kiungo wao wa zamani wa kikosi hicho, Benard Morrison, wakati kamati ya maadili ya TFF ikiwa inaendelea na kazi yake.

Katika taarifa yake ya juzi, Kamati ya Maadili ilisema kwamba katika kikao chake cha Juni 23, kiliridhishwa na sababu zilizotolewa na Mwakalebela, hivyo kuondolewa kifungo na faini vilivyokuwa vikimkabili.

Lakini kitu kinachoonekana kwa sasa hadi kufunguliwa kwa Mwakalebela ni kelele zilizopazwa na wadau na wabunge, ambao walidai kuwa adhabu hiyo ni kuikomoa Yanga na kiongozi huyo.

Mapema mwezi uliopita, mmoja wa wabunge waliochangia bajeti ya Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo juu ya adhabu zilizokuwa zikitolewa na shirikisho hilo.

Lakini pia, uwepo wa mkutano mkuu wa Yanga wa Jumapili hii na mchezo wa watani wa jadi, zinatajwa kuwa miongoni mwa sababu za kufunguliwa kwake.

Akizungumza juzi, mchambuzi wa soka nchini, Oscar Oscar alisema kufunguliwa kwake kumekuwa jambo zuri na pia la funzo kwa viongozi wa soka nchini waliopewa dhamana ya kuongoza klabu kama Yanga.

Oscar alisema ni kweli kuwa kiongozi huyo alikosea, lakini bado kuna udhaifu mkubwa katika sheria zinazoongoza soka nchini, hivyo kuna kila sababu ya kuliangalia upya suala hilo.

“Limekuwa jambo zuri, lakini ni kweli kwamba Mwakalebela alikosea na ni suala la kujifunza ukiwa na dhamana ya kuongoza klabu kubwa, lakini udhaifu katika kanuni zetu pia ni jambo jingine la kuliangalia,” alisema.

Wakati Yanga ikishangilia kuachiwa huru kwa kiongozi wao, kikosi cha miamba hiyo leo kitakuwa na kazi ngumu katika mchezio wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), itakapocheza na Biashara United kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

Wakati hesabu za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu zikionekana kuwa ngumu kutokana na Simba kuwa katika nafasi nzuri, Kombe la FA ndilo pekee ambalo angalau linaweza kuifanya Yanga kumalize msimu ikiwa imetwaa taji.

Kiwango bora cha safu ya ushambuliaji ya Yanga katika siku za hivi karibuni kinaonekana kinaweza kuwa silaha muhimu kwa timu hiyo inayonolewa na kocha Nasreddine Nabi katika mchezo wa leo.

Rekodi ya michezo saba iliyozikutanisha timu hizo katika Ligi Kuu na FA inawapa imani Yanga kuibuka na ushindi leo. Yanga imeshinda mechi tano, sare moja na kupoteza moja.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz