Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilele cha Mwananchi Day kuweka historia kwa Mkapa

Mwananchi Pic Data Kilele cha Mwananchi Day kuweka historia kwa Mkapa

Thu, 26 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. AGOSTI 29, ndio kilele cha wiki ya Mwananchi katika dimba la Benjamin Mkapa kwa wapenzi na mashibaki wa timu ya Yanga kwenda kushuhudia burudani mbalimbali katika dimba hilo.

Katika siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo kutambulishwa kwa wachezaji wapya ambao wamesajiliwa msimu huu, waliokuwepo katika kikosi msimu uliopita pamoja na benchi la ufundi.

Burudani nyingine ambayo mashabiki wa Yanga na wapenzi wa soka nchini wanaisubiri kwa hamu ni kutoka kwa msanii nguli wa muziki wa dansi kutoka DR Congo, Koffi Olomide.

Katika orodha hiyo wa wasanii watakuwepo ni Billnass, Gnako, Chege na Mwanadada Nandy, Mh Temba, Baba Levo pamoja na msanii wa singeli Mzee wa Bwax.

Mbali ya burudani hizo zote hitimisho lake jioni itachezwa mechi ya kimataifa ya kirafiki ambayo Yanga watajipima ubavu dhidi ya miamba ya Ligi Kuu ya Zambia, Zanacco FC.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz