Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kila la heri Taifa Stars

F8a2ad7033c4f926bd9ddb0b6c25b118 Kila la heri Taifa Stars

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

LEO wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), watakuwa na kibarua kigumu cha kusaka pointi tatu dhidi ya Namibia katika mchezo wa pili wa Kundi D katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani (Chan) zinazoendelea Cameroon.

Mchezo huo utachezwa kuanzia majira ya saa 4:00 usiku jijini Limbe, Taifa Stars wanahitaji ushindi kufuta makosa yaliyowafanya kwa kupoteza mechi ya kwanza baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Zambia.

Ni wazi Watanzania na wadau wote wanaitakia timu hiyo kila la heri ili ifanye vyema katika mchezo huu na hivyo, waweze kujitengenezea mazingira ya kukalia nafasi ya juu kwenye kundi hilo, linaloongozwa na Guinea yenye pointi tatu sawa na Zambia wanaoshika nafasi ya pili wakitofautiana kwa mabao ya kufunga.

Wakati Taifa Stars wanashika nafasi ya tatu wakiwa hawana pointi hata moja sawa na Namibia wanaoshika mkia kwenye kundi hilo wakitofautiana kwa mabao ya kufungwa, Stars wenyewe walifungwa 2-0 na Zambia.

Ugumu wa mchezo huo unatokana na vikosi vyote kupoteza michezo yao ya raundi kwanza, ambapo Namibia walifungwa mabao 3-0 dhidi ya Guinea, hivyo kila upande utaingia uwanjani kwa lengo la moja tu, la kupata ushindi.

Ni mchezo mgumu, lakini Kocha Etienne Ndayiragije, ameishabaini upungufu uliokuwapo katika mchezo uliopita, hivyo Watanzania hasa washabiki wa soka tunategemea ataingia na mbinu ya kuwadhibiti kwa kucheza kwa kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza.

Watanzania wengi wanahitaji kuona kikosi hicho kinakwenda hatua ya mbali zaidi, jambo ambalo benchi la ufundi wanajua shahuku hiyo, hivyo watakuwa wameongea na wachezaji na kuwapa mbinu anuai za kusahihisha makosa waliyofanya katika mechi ya kwanza.

Mchezo wa leo una umuhimu mkubwa wa kuamua hatima ya kusonga au kubaki, kwani katika kila kundi timu mbili zitakazoongoza kwa idadi, zinasonga hatua ya robo fainali.

Katika mchezo uliopita, wachezaji wa kikosi hicho walionekana kukosa hali ya kujiamini na kushindwa kutumia nafasi chache walizopata kufunga mabao.

Mchezo dhidi ya Namibia kama Stars watakuwa wamejipanga vyema, unanaweza kuibuka na ushindi isipokuwa, katika kikosi hicho kunapaswa kuwapo mchanganyiko wa wachezaji vijana na wazoefu.

Katika mchezo uliopita, kuna wakati wachezaji wa kikosi hicho walikuwa wanaonekana kukosa watu wa kuwaongoza kiasi cha kuwafanya kushindwa kufanya uamuzi haraka wanapoingia katika maeneo ya hatari.

Wapo wachezaji wengi wazoefu. Kwa mfano, John Bocco, Deus Kaseke, Said Ndemla na Erasto Nyoni. Huu ni wakati wa kuwapa majukumu katika mchezo huo kutokana na umuhimu wake.

Kwa mtanzamo wangu, huu si wakati wa kulikosoa benchi la ufundi baada ya kupoteza mchezo wa kwanza, bali tunatakiwa kuwaunga mkono kwa kupambana na watakuwa na moyo wa kujipanga upya kuona wanatufuta machozi kupitia mchezo wa leo.

Michuano hiyo inashirikisha timu 16 zilizopangwa kwenye makundi manne.

Kila kundi lina timu nne ambapo watacheza michezo mitatu na washindi wawili watakaoongoza kwa idadi ya pointi kwa michezo yote ya jumla, watasonga hatua inayofuata.

Tanzania inashiki kwa mara ya pili mashindano hayo yaliyoanzishwa mwaka 2009. DR Congo wamechukua mara mbili huku Morocco na Tunisia wakichukua mara moja moja.

Chanzo: habarileo.co.tz