Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kila kona Makambo...

32025 Pic+makambo TanzaniaWeb

Mon, 17 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ukisikia Makambooo ujue imo. Kama ukitaka usalama mkabe hadi mwamuzi apige filimbi ya mwisho, vinginevyo hakuachi salama.

Hali hiyo imewakuta Ruvu Shooting jana baada ya kujisahau na akawatungua dakika za majeruhi ikibakia sekunde 25 tu mpira kumalizika.

Hilo ni bao la tisa la mchezaji huyo akimkuta Eliud Ambokile wa Mbeya City.

Ulikuwa mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajib akajitwika na kuuzamisha mpira kimiani na kuipa Yanga pointi 44 kileleni.

Awali Yanga ilikuwa ya kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 11 lililofungwa na Amiss Tambwe akimalizia kazi ya Heritier Makambo aliyemchambua kipa wa Ruvu Shooting, Abdallah Rashid.

Dakika 19 Dilunga alipiga kisigino ndani ya 18 na kukutana na Fuluzulu Maganga lakini hata hivyo, mchezaji huyo alidondoshwa ndani ya eneo la hatari lakini refa alionyesha mpira kuendelea na shambulizi hilo halikuwa na faida kwao.

Dakika 31 Maganga aligongeana pasi na Shaaban Msala na kuwaacha mabeki wa Yanga na kisha kuingia ndani ya 18 na kupiga shuti ambalo lilitinga wavuni na kumfanya kipa Ramadhan Kabwili asijue nini cha kufanya. Upande wa kushoto wa beki ya Yanga alipokuwa anacheza Haji Mwinyi, Ruvu Shooting walikuwa wakitumia kama njia kwani mchezaji wao, William Patrick alikuwa msumbufu na kumfanya Mwinyi asipande kabisa kupeleka mashambulizi. Beki Andrew Vincent ‘Dante’ alifanyiwa mabadiliko dakika 41 baada ya kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kuonekana kupata maumivu na nafasi yake ilichukuliwa na Cleofas Sospeter.

Kipa wa Shooting alionekana kuigiza kuumia na mwamuzi Fikirini Yusuph alimpa kadi ya njano dakika 78 na mpira ulipoanza zilipigwa gonga na mpira wa mwisho ukamkuta kiungo Feisal Salum aliyepiga shuti kali na kutinga wavuni na kuifanya Yanga kuwa mbele kwa 2-1. Shooting nao licha kwamba walikuwa nyuma kwa 2-1 walizidi kusongesha mashambulizi na dakika 83 Said Dilunga alifanyiwa madhambi na Sospeter nje ya 18 na mpira ulikuwa faulo ambayo ilipigwa na Amis Tambwe aliunawa mpira ndani ya 18 na kuwa penalti iliyopigwa na Dilunga mwenyewe na kutinga wavuni na kufanya matokeo yawe 2-2.

Ndipo ilipogota dakika za majeruhi, Yanga ilipata faulo baada ya Paul Godfrey kufanyiwa madhambi nje ya 18 na ilipigwa kifundi na Ajib akimwangalia Makambo ambaye naye aliutumbukiza wavuni.



Chanzo: mwananchi.co.tz