Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikwete: Yanga waliponialika nilijuliza mara mbili

Jk Data Kikwete: Yanga waliponialika nilijuliza mara mbili

Mon, 28 Jun 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema alipopata mualiko wa kuhudhuria na kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa klabu ya Yanga, alijiuliza aende au asiende.

Kikwete amebainisha hayo kwenye mkutano huo na kueleza kwamba, alirudhia baada ya kuhakikishiwa mkutano ni wa amani na baada ya kuzisoma ajenda.

"Nilijiuliza niende, nisiende maana mikutano ya aina hii ina mambo mengi," amesema Rais huyo wa awamu ya nne

Kikwete amewashauri wanachama wakosoaji kuwa wasikosoe kwa nia ya kubomoa, bali kwa kujenga.

‘”Msiache kusema kwenye mkutano mkuu kama huu na kulalamika vijiweni, huo ni usengenyaji na unaleta mpasuko klabuni.

"Watu wa namna hii msiwaendekeze, watu wa aina hii waambieni ukweli," alisema.

Related Kikwete ndani mkutano wa Yanga



JK, Manji wafunika mkutano mkuu Yanga


Manji atua, apagawisha wanachama mkutano Yanga


Katibu mkuu TFF akumbana na zomeazomea mkutano Yanga
Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz