Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikapu yapania makubwa Kanda ya Tano Afrika

8927 KIKAPU+PIC TZW

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha . Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), limesema limejipanga vyema kutwaa ubingwa wa mashindano ya Kanda ya Tano Afrika kwa vijana chini ya miaka 18.

Rais wa TBF Phares Magesa alisema mkakati ni kutwaa ubingwa unaoshikiliwa na Misri, katika mashindano hayo yaliyopangwa kuanza Juni 17 hadi 22 Dar es Salaam.

Magesa alisema timu hiyo inatarajiwa kuingia kambini Juni 12 kujiandaa kushiriki mashindano hayo.

Akizungumzia timu kuchelewa kuingia kambini, Magesa alisema wachezaji wengi ni wanafunzi na wanatoka mikoa mbalimbali nchini, hivyo walisubiri shule kufungwa.

“Tuna ahadi nyingi za wadau kutusapoti, lakini baadhi hawajatekeleza ndio maana hata baada ya shule kufungwa tumeshindwa kuwaingiza wachezaji kambini kwa wakati,” alisema Magesa.

Tanzania inayoandaa mashindano hayo kwa mara ya kwanza, itawakilishwa na timu mbili za wasichana na wavulana wanaounda timu za Taifa. Kamishna wa watoto na shule wa TBF Abdallah Mpogole alisema wachezaji wana morali ya kufanya vyema katika mashindano hayo.

Nchi zitakazoshiriki ni Kenya, Uganda, Burundi, Misri Sudan, Sudan Kusini, Eritrea, Djibout, Ethiopia na Rwanda.

Chanzo: mwananchi.co.tz