Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikapu kutembeza bakuli la fidia

Fri, 2 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa amefunguka kuhusu madai ya kushindwa kumrejeshea gharama ambazo mchezaji wa timu ya Taifa, Murshid Mudricat alipoitwa kwenye timu ya taifa.

Mchezaji huyo anayesoma Marekani alikuwa ni miongoni mwa nyota wanne wa kimataifa walioitwa kuitumikia timu ya Taifa kwenye mashindano ya Afrika ingawa watatu walikwama kuja kutokana na TBF kukosa fedha za kuwagharamia.

Inadaiwa Mudricat alitumia gharama zake kuja kuitumikia timu ya Taifa alidai uongozi wa TBF uliahidi kumrejeshea fedha hiyo dola 1600, lakini imekuwa tofauti baada ya mashindano kumalizika.

Akizungumzia madai hayo, Magesa alidai mchezaji huyo aliamua kujitolea kujigharamia ili aitumikie timu ya Taifa na hawakukubaliana wamrudishie gharama zake, lakini baada ya mashindano ndipo yakaibuka madai hayo.

"Hatuna namna, labda tufanye harambee kumchangia, lakini kwa sasa Shirikisho haliko vizuri kiuchumi," amesema.

Amesema wanafikiria kutumia njia hiyo ili kumalizana na mchezaji huyo japo TBF haikuwa na makubaliano ya kumlipa Mudricat.

"Tuliwazuia wachezaji wote wa kimataifa, ambao Mudricat na Hasheem Thabeet walikuwa wakitokea Marekani, mwingine Canada na mwingine Ufilipino.

"Lakini Mudricat akasema yeye atakuja kwa kutumia gharama zake, hatukuweza kumzuia kwa kuwa alionyesha kuwa na mapenzi na timu ya Taifa, lakini baada ya mashindano ndipo anadai tulikubaliana tumrejeshee fedha zake, kitu ambacho si kweli," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz