Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikapu Mwanza wamlilia JPM

B200337f45ed43c43ea57ab625ce833b.jpeg Kikapu Mwanza wamlilia JPM

Sat, 20 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

CHAMA cha mpira wa kikapu mkoa wa Mwanza (MRBA) kimepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Rais ya awamu ya tano John Magufuli aliefariki dunia Jumatano ya wiki hii.

Hayo yalisemwa jana na Katibu mkuu wa chama hicho Haidari Abdul na kuongeza kuwa wakati wa Magufuli mpira wa kikapu nchini ulipata heshima kubwa pamoja na kupatikana kwa udhamini katika mashindano ya kombe la taifa yaliyofanyika mwaka jana jijini Dodoma.

Alisema bila uongozi wa rais Magufuli viongozi wa mpira wa kikapu wasingeweza kupata udhamini. Alisema pia katika uongozi wake wameweza kujenga viwanja viwili vya mpira wa kikapu katika eneo la Mirongo wilayani Nyamagana na Sabasaba katika kata ya Ilemela.

Kwa upande wake,rais wa mpira wa kikapu nchini (TBF) Phares Magesa alisema rais Magufuli alikuwa na mpango wa kujenga uwanja wa ndani wa michezo jijini Dodoma.

Amewaomba viongozi waliopo madarakani wasaidie kutimiza malengo ya rais Magufuli kwa kutafuta wafadhili ili watimize malengo ya ujenzi mbali mbali ya viwanja.

“Viwanja vingi vimejengwa haswa katika mikoa mbali mbali ikiwemo uwanja wa Kikapu wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Manyara pia uwanja ulijengwa pamoja na Arusha katika eneo la Ngarenaro uwanja ulijengwa,’’ alisema Magesa.

Magesa alisema rais Magufuli alikuwa akipenda timu zifike mbali katika mashindano mbali mbali ndio maana akatenga bajeti kwajili ya timu za Taifa.

Alisema katika miaka ya nyuma timu za Taifa zilikuwa zinaachiwa kwa vyama vya michezo tu lakini wakati wa Rais Magufuli alisaidia.

Alisema wakati wa rais Magufuli katika mchezo wa mpira wa kikapu wamefanikiwa kushiriki mashindano mbali mbali.

Alisema mwaka 2018 timu ya Taifa ya vijana ilishiriki mashindano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 18. Pia timu ya taifa chini ya umri wa miaka 16 ilifuzu katika mashindano ya kanda.

Alisema mwaka 2019 waliandaa mashindano ya ligi ya Afrika kwa ushirikiano kutoka NBA na Shiriksho la mpira wa kikapu Duniani(FIBA).

Chanzo: www.habarileo.co.tz