Dar es Salaam. Klabu ya Simba, imetangaza viingilio katika siku yao maalumu ya Simba Day, Agosti 8 ambayo wataitumia kufanya utambulisho wa kikosi chao kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana.
Msemaji wa timu hiyo, Haji Manara ametengaza viingilio hivyo kwa kusema wamepanga vya kawaida kwa lengo la kutoa nafasi kwa mashabiki wa timu hiyo ili wajitokeze kwa wingi.
“Viingilio kwa viti vya mzunguko ni 5,000 kwa upande wa VIP ‘A’ ni 20, 000 na VIP ‘B’ ni 15, 000. Ticketi zitaanza kuuzwa Jumanne na tutaangaza mahali ambapo zitapatikana,” alisema Manara.
Katika siku hiyo ya Simba Day, Manara alisema kutakuwa na burudani kabambe kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiwemo wa muziki wa Bongo Fleva ambao Mwasiti na Tunda Man , Sengeli michano ambaye ni Msaga Sumu na Bongo Movie akiwemo Monalisa na JB.