Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kifukwe: Fainali? Simba wasahau

Kifukwe Pic Data Kifukwe: Fainali? Simba wasahau

Sun, 30 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MWENYEKITI wa zamani wa Yanga na kigogo wa kundi la Yanga Family, Francis Kifukwe amesema kama Simba na Yanga zitacheza fainali ya FA basi, Simba isitarajie ubingwa.

Simba imepangwa kucheza na Azam kwenye nusu fainali ya FA huku Yanga ikikutana na Biashara na watani hao wakishinda mechi zao wanakutana fainali.

“Simba wanafikiri Yanga tunawaogopa, lakini haiko hivyo kabisa, kama hawataki kuamini basi tucheze nao mechi ya kirafiki kabla ya Julai 3,”alitania Kifukwe ambaye amekaa kwenye kamati mbalimbali za Yanga miaka mingi.

Kiongozi huyo ambaye amehusika kwenye mafanikio ya Yanga mwanzoni mwa miaka ya 2000, alisema hana shaka Yanga itatinga fainali ya FA, hivyo Simba asijekutafuta sababu akafungwa na Azam ili haikwepe Yanga.

“Tunamuombea mtani tukutane naye kwenye fainali, hapo ndipo hatajua hajui,” alisema Kifukwe.

Alisema hata kilichotokea Mei 8 hadi mechi yao kuahirishwa, Yanga haikumuogopa Simba, ndiyo sababu ilipeleka timu.

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amebainisha kwamba malengo ya klabu yao ni kutwaa ubingwa wa FA na Ligi kuu kwa mara nyingine.

“Kwa ubora wa kikosi chetu, namna tulivyojipanga na rekodi tuliyonayo, hakuna kitakachotukwamisha kutwaa ubingwa wa FA na Ligi pia,” alisema

Alisema watacheza nusu fainali ya FA wakiiheshimu Azam kama timu bora, lakini kwa malengo ya ushindi na kutinga fainali.

“Kwenye fainali yoyote aje, tutamfunga na kutwaa ubingwa ili kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa wa FA na Ligi,” alisema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz