Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kifua, mafua tishio kwa wachezaji Simba

Ugonjwa Pic Data Kifua, mafua tishio kwa wachezaji Simba

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mkoani Kagera Matola amesema wachezaji wengi wanakabiliwa na ugonjwa huo ambao haujulikani chanzo chake ingawa madaktari bado wanafanya vipimo mbali mbali kujua chanzo

“Nashkuru Mungu tumeweza kufika salama jana japokuwa tumekuwa na changamoto kidogo baadhi ya wachezaji nafikiri karibu robo tatu wamekuwa wakiugua mafua na kifua na homa za hapa na hapa sijui ni kutokana na hali ya hewa au ni nini na baadhi ya benchi la ufundi” amesema Matola na kuongeza

“Mpaka sasa hatujui itakuwaje kwani hatujui chanzo na tumeacha madaktari wafanye vipimo na baadae tujue nini tatizo kwani hata mimi na baadhi ya watu wa benchi la ufundi wanaumwa”

Kwa upande wake Francis Baraza ambae ni Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema timu Yake pia inakabiliwa na tatizo hilo kwani daktari wa timu na kocha Msaidizi wanaumwa

“Hili tatizo pia kwetu lipo tumetokea kwenye mchezo dhidi ya Azam baadhi ya watu wa benchi akiwemo daktari na kocha msaidizi wanaumwa nadhani ni suala la mabadiliko ya hali ya hewa". amesema Baraza

Related Morrison, Bwalya kuikosa Kagera Pablo kufyeka watatu SimbaSimba watamenyama na Kagera Sugar hapo kesho Desemba 18 katika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz