Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kidao afunguka kesi ya vigogo TFF

28284 Tff+pioc TanzaniaWeb

Thu, 22 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kidao Wilfred (41) ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa tangu awe Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF mwaka 2013, mpaka 2017, hajawahi kuona maombi kuhusu taasisi hiyo kukopeshwa fedha na mtu binafsi.

Kidao aliyaeleza hayo jana, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard Mashauri wakati akitoa ushahidi katika kesi inayomkabili aliyekuwa rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake wanne.

Shahidi huyo wa nane wa upande wa mashtaka alieleza hayo mahakamani hapo, baada ya kuulizwa na wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Leonard Swai.

Swai alimuuza Kidao akiwa Mtendaji na Katibu Mkuu wa TFF ni mara ngapi aliwahi kuona maombi ya mshtakiwa wa kwanza ya kuikopesha fedha taasisi hiyo nyeti katika mchezo wa soka nchini.

Alidai utaratibu wa TFF inapohitaji kukopa fedha inaomba ridhaa ya kamati ya utendaji kwa mujibu wa kanuni za fedha za shirikisho hilo.

Alisema maombi hayo huwasilishwa kwa njia ya vikao na kuwatumia wajumbe waraka kwa barua pepe ambapo hujibu kwa kukubali ama kukataa.

Kidao alidai akiwa ndiye Katibu Mkuu wa TFF hajawahi kupata madai yoyote ya marejesho.

Shahidi huyo aliendelea kutoa ushahidi alidai masuala yote yanayohusu fedha yanapaswa kupitishwa na Kamati ya Utendaji ya TFF na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu.

Baada ya shahidi huyo wa upande wa mashtaka kueleza hayo, kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, Richard Rweyongeza alimuuliza unakumbuka kuna kipindi akaunti ya TFF ilifungiwa.

Katibu Mkuu huyo alidai kuwa mara nyingi akaunti ya TFF imekuwa ikipata matatizo ya kufungiwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz