Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kichuya afunga goli Bara ikipita miezi 26

92368 Kichuya+pic Kichuya afunga goli Bara ikipita miezi 26

Tue, 16 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KIUNGO wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, Shiza Kichuya amefunga bao la kwanza katika ligi hiyo baada ya miezi 26, imefahamika.

Bao la dakika ya 11 lililofungwa na kiungo huyo kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara juzi, ndio bao lake la kwanza msimu huu, baada ya kurejea klabuni hapo.

Mara ya mwisho Kichuya kufunga bao ilikuwa ni Februari 26, mwaka 2018 kwenye uwanja huo huo jijini Dar es Salaam akiwa na timu yake ya Simba illipocheza dhidi ya Mbao FC, mechi ya Ligi Kuu msimu wa 2017/18.

Kwenye mechi hiyo, Kichuya alifunga bao la kwanza dakika ya 37, Simba ikishinda mabao 5-0, mengine yakifungwa na Emmanuel Okwi aliyepachika mawili, Erasto Nyoni na Nicolaus Gyan.

Ni msimu ambao kiungo huyo alimaliza akiwa na mabao saba ya kufunga.

Januari 2019, Simba ilimuuza kiungo huyo katika klabu ya Pharco ya Daraja la Pili nchini Misri ambayo nayo ilimtoa kwa mkopo kwenye klabu ya Ligi Kuu nchini humo ENPPI.

Hata hivyo hakuwa kwenye wakati mzuri nchini humo na Simba ilimsajili tena kwenye kipindi cha dirisha dogo msimu huu.

Pamoja na kusajiliwa alionekana kutokuwa kwenye kiwango kizuri, kiasi cha kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza cha vinara hao wa Ligi Kuu Bara.

Kichuya alianzishwa kwenye mechi ya Jumapili dhidi ya Ruvu Shooting na kuonyesha kiwango kizuri kiasi na kufunga bao lake la kwanza na kwa klabu yake, ingawa baadaye alitoka na kumpisha, Francis Kahata kwenye mechi ambayo iliisha kwa sare ya bao 1-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live