Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kichapo chaiharibia Dodoma Jiji

5b9552ea9f0ecede6bc59edd1ee4b3f0.jpeg Kichapo chaiharibia Dodoma Jiji

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata amesema kichapo cha bao 1-0 walichokipata kutoka kwa Ihefu, kimeharibu hesabu zao za kuendelea kusogea juu ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuweka hai matumaini ya kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Highland Estate, Mbarali, Mbeya, bao pekee la Ihefu lilifungwa na mshambuliaji Emmanuel Simchimba dakika ya 18 kwa mkwaju wa penalti baada ya beki wa Dodoma Jiji, George Wawa kuunawa mpira ndani ya boksi na mwamuzi Ludovick Charles, kutoa penalti kwa wenyeji.

Akizungumza na gazeti hili baada ya mchezo huo Makata, alisema mchezo huo ulikuwa muhimu kwao kushinda kutokana maandalizi waliyofanya, lakini kupoteza ni sehemu ya mchezo hivyo wanajipanga kwa ajili ya michezo ijayo ya ligi kuangalia kama wanaweza kutimiza malengo yao.

“Tulipaswa kushinda mchezo huu ili kutanua wigo wa pointi kati yetu na anayetufuatia ili kuongeza kasi ya kujihakikishia nafasi nne za juu, lakini naamini kwa michezo iliyosalia tutaweza kufanikisha malengo yetu,” alisema Makata.

Dodoma Jiji inashika nafasi ya nane ikiwa na pointi 40 baada ya kushuka uwanjani mara 30, huku Ihefu ikifikisha pointi 34 na kupanda hadi nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz