Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibarua cha Nuno Spurs mashakani

Nuno Espirito Santo Tottenham 1514292 Kocha wa Tottenham Hotspurs ,Nuno Espirito Santo

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Kibarua cha kocha wa Tottenham Hotspurs ,Nuno Espirito Santo kipo mashakani kufuatia kipigo cha bao 3-0 walichokipokea kutoka kwa Manchester United Jumamosi iliyopita kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Mwenyekiti wa Tottenham Hotspurs, Daniel Levy amekutana na Mkurugenzi wa soka Fabio Paraciti kujadili mwenendo wa Kocha huyo.

Kocha huyo wa zamani wa Wolves alisaini Mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha Tottenham Hotspurs mnamo mwezi Juni mwaka huu.

Licha ya kuanza vizuri msimu, Spurs imepoteza mechi tano kati ya saba za Ligi Kuu ya Ungereza, wakikamata nafasi ya nane kwenye msimamo wakiwa nyuma kwa alama kumi dhidi ya vinara Chelsea.

Iwapo Levy atafanya maamuzi, huenda aliyekuwa kocha wa AS Roma, Paulo Fonseca ambaye amekuwa akiwindwa kwa muda mrefu na klabu hiyo.

Chanzo: eatv.tv