Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Malinzi, wenzake kusikilizwa kwa siku tatu

34536 Pic+malinzi Tanzania Web Photo

Wed, 2 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake itasikilizwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia Januri 16, 2019.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga ambao wanakabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo utakatishaji fedha Dola 173,335 za Marekani.

Wakili wa Serikali, Neema Mbwana ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Januari 2, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na kumbukumbu inaonyesha kuwa tayari tarehe ya kuendelea kusikilizwa imeshapangwa.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mashauri amesema kesi hiyo itaendelea na ushahidi Januari 16, 17 na 21 mwaka huu.

Katika kesi ya msingi, inadaiwa Juni 5, 2017, maeneo ya jiji la Dar es Salaam, Malinzi na Selestine walighushi nyaraka ya maazimio ya kamati ya utendaji kwa lengo la kuonyesha kuwa kamati hiyo ya TFF imelenga kubadili mtia saini wa shirikisho hilo katika akaunti za benki kutoka kwa Edgar Masoud kwenda kwa Mwanga.

Inadaiwa kuwa Malinzi, Mwesigwa na Nsiande walitakatisha Dola 173,335 za Marekani na wako mahabusu kwa sababu mashtaka yao hayana dhamana kisheria.



Chanzo: mwananchi.co.tz