Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenyatta azindua awamu ya Kwanza ya Ujenzi wa Uwanja wa Kisasa

UHUNYE FUNGUA STADI.jpeg Kenyatta azindua awamu ya Kwanza ya Ujenzi wa Uwanja wa Kisasa

Sat, 26 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta amezindua mpango wa awamu ya kwanza wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo mbalimbali unaoendelea katika barabara ya Ngong na kupewa jina la Jamhuri Sports Complex.

Uzinduzi huo, umefanyika Ijumaa Machi 25, ambapo unakusudiwa kuwa na viwanja takribani vitano vya michezo hiyo tofauti mchezo wa raga, michezo ya kukimbia, viwanja vitatu vya kandanda, maeneo ya kupaki magari, sehemu za kucheza watoto.

Mbali na viwanja hivyo, mpango huo unakusudia kujenga sehemu za kupatia burudani, chakula sehemu za kuabudu ikiwa ni sehemu ya kuuweka uwanja kuwa wa kisasa zaidi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Michezo Amina Mohamed amesema kuwa kama ambavyo kuna nyota wamefanikiwa kulitangaza taifa kimataifa katika mazingira magumu basi uwepo wa mazingira wezeshi kwa sasa utaenda kuinua zaidi vipaji wachezaji.

Eneo la uwanja hilo lenye zaidi ya hekari 79, unatajwa kuwa baada ya kukamilika ujenzi wake utakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Kenya na kukuza vipaji vya wanamichezo nchini humo hata wale ambao watahitaji kwenda kupata burudani kabla, wakati na baada ya mchezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live