Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Keita afafanua jina la Deco

17678 Pic+keita TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

London, England. Kiungo mahiri wa Liverpool, Naby Keita ‘Deco’ raia wa Guinea, amefichua kuwa jina la Deco ni la utani na alipewa wakati mdogo na baba yake mzazi.

Alisema kuwa alipewa jina hilo kutokana na baba yake kukunwa na kipaji chake na kumfananisha na kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa uwanjani na staa wa kibrazil aliyechukua uraiwa Ureno, enzi hizo akiitumikia Chelsea.

Kiungo huyo amejiunga na Liverpool akitokea timu ya Leipzig ya Ujerumani na tayari ameichezea timu yake mpya mechi nne kati ya tano za ligi kuu ilizocheza msimu huu ikishinda mechi zote.

Alisema hata yeye wakati anaikua alikuta watu wanamuita Deco na hakujua kutofautisha jina hilo na majina yake mengine hadi aliposimuliwa na baba yake Sekoe asili ya jina hilo. 

Keita alifichua kuwa pamoja na kuwa na kipaji cha soka baba yake hakumruhusu kwenda kucheza na watoto wenzake mitaani badala yake alikuwa akimlazimisha kukaa ndani.

“Nilikuwa naenda kucheza kwa kutoroka nilipigwa lakini nilitoroka tena sikua najali ningeweza kutoka hata kama imebakia nusu saa kabla ya jua kuzama nilikuwa sijali nilikuwa natamani kucheza hata kama ni dakika moja,” alisema.

Alisema baada ya kuonyesha kipaji kikubwa katika umri mdogo alitakiwa kwenda Ufaransa kuendelea kipaji chake na huko alikutana na Kocha wa zamani wa Liverpool, Gerard Houllier, ambaye ndiye aliyemfikisha hapo alipo leo.

Chanzo: mwananchi.co.tz