Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kavila ampa dili Ndemla

9512 Pic+ndemla TZWeb

Tue, 19 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kiungo mkongwe wa Kagera Sugar, George Kavila amemshauri Said Ndemla wa Simba kutoogopa kutafuta maisha mengine ya soka nje ya mipaka ya Tanzania.

Kavila amewataka wanaomsimamia mchezaji huyo kutomchelewesha kumtafutia soko nje ya nchi, ili kipaji chake kikaongezewe mbinu nyingine ambazo zitafaidisha kikosi cha Taifa Stars.

"Ndemla ana kipaji kikubwa na ndio maana Simba anaweza akakaa benchi akija kupangwa anastajabisha wanalijua soka, asiangalie sifa anazopata kwa mashabiki wake bali maisha ya badaae.

"Unajua kuna mchezaji ukimwangalia unajua amebeba utajiri mguuni mwake ila anakuwa hajaona njia ya kuziona pesa hizo kwa macho na hilo ndilo ninaloliona kwa huyo dogo Ndemla," anasema Kavila.

Kavila anasema kama mkongwe ana wajibu wa kuwakumbusha chipukizi kutojisahau na kujua soka lina kipindi kifupi, hivyo wawe waangalifu kutochezea muda.

"Mfano mzuri ni mchezaji wa umri wao Mbwana Samatta anafanikiwa kung'aa nje kwa kuwa alifanya uamuzi wakati sahihi na hakutaka kupoteza muda na ndio maana kila anayemuona anatamani angekuwa na mafanikio kama yake."

Chanzo: mwananchi.co.tz