Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katwila ajivunia vipaji lukuki Mtibwa Sugar

KATWILO.webp Katwila ajivunia vipaji lukuki Mtibwa Sugar

Mon, 27 Apr 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila, amesema klabu hiyo ni chuo cha kuzalisha vipaji na ana imani ya kukiboresha kikosi chake endapo baadhi ya nyota wake watapata nafasi ya kusajiliwa na timu zingine.

Kauli hiyo imekuja baada ya kuzagaa kwa taarifa kuwa kuna baadhi ya nyota wake akiwamo Salim Kihimbwa na Abdulhalim Humud, kutajwa kutakiwa na Yanga inayowania kuinasa saini yake kwa ajili ya msimu ujao.

Katwila ameliambia gazeti hili kwamba, hana tatizo wala hofu juu ya nyota wake hao kutakiwa na timu zingine kutokana na kujawa na imani ya kupata mbadala wao kutokana na timu yao kuwa na hazina kubwa ya vijana.

Alisema kuwapo kwa hazina ya nyota wengi katika klabu hiyo kwa upande wa timu ya vijana, kunamfanya ajivunie na kutokuwa na presha ya baadhi ya nyota wake kutajwa kutakiwa na timu nyingine.

"Kwa upande wangu sina hofu na wachezaji hao au wengine kutakiwa kwenda kupata ushindani katika timu zingine, kwa sababu kwetu ni chuo, hivyo kama itatokea wakaondoka, nitapata wachezaji ambao wataziba nafasi zao," alisema Katwila.

Alisema kwa sasa bado wapo kimya juu ya nafasi watakazosajili kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa kuendelea na baadhi ya nyota wake wa kikosi cha kwanza wanaotajwa kutakiwa na timu nyingine.

Ligi Kuu Bara imesimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona na wachezaji wapo nyumbani wakiendelea kufanya mazoezi binafsi pamoja na kuchukua tahadhari dhidi maambukizo ya virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live