Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katiba kutawala Mkutano Mkuu TFF

39678 Tff+pict Katiba kutawala Mkutano Mkuu TFF

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Wakati Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukifanyika leo jijini Arusha, ajenda ya marekebisho ya Katiba ya Shirikisho hilo inaweza kuacha kilio au kicheko kwa baadhi ya wadau wa soka nchini.

Ajenda hiyo namba 12 ni mwa ajenda 14 zitakazofanyiwa kazi katika mkutano huo utakaofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC) kilichopo jijini hapa huku mgeni rasmi akiwa mkuu wa Mkoa huu Mrisho Gambo.

Kupitia ajenda hiyo, wajumbe wa Mkutano Mkuu watakuwa na fursa ya kupitisha au kugomea mabadiliko ya vipengele kadhaa kwenye katiba ya TFF ya mwaka 2013 ambayo ilifanyiwa marekebisho kadhaa mwaka 2015.

Mara kwa mara marekebisho ya katiba zinazoongoza taasisi za kimpira hugusa kwenye masuala kama vile namna ya upatikanaji wa viongozi kama Rais, Makamu wa Rais, wajumbe wa Kamati ya Utendaji pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu, muundo wa uongozi pamoja na mamlaka na mipaka ya kamati na vyombo mbalimbali vinavyoendesha taasisi husika.

Ni wazi kwamba marekebisho ya Katiba ya TFF leo, kwa kiasi kikubwa yatagusa katika maeneo tajwa jambo ambalo linaweza kuwa na manufaa kwa watu fulani huku likiwatega wengine. Kuna wale ambao huenda wakanufaika na marekebisho hayo.



Chanzo: mwananchi.co.tz