Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaseke: Makocha Everton wamenipa faraja

8913 Pic+kaseke TZW

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

WINGA wa Singida United, Deus Kaseke amefarijika kuchaguliwa mchezaji bora wa mechi yao ya mshindi wa tatu dhidi ya Kakamega Homeboys na kusema kitendo hicho kimemfanya ahamasike zaidi na kazi yake ya soka.

Singida imeishida Kakamega Homeboys kwa mikwaju ya penalti 4-1 na kuibuka washindi wa tatu wa michuano ya SportPesa Super Cup 2018.

Kaseke ambaye alicheza kwa dakika zote kwenye mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 na kisha jopo hiyo la makocha kutoka Everton kumchagua mchezaji bora wa mchezo.

"Ni jambo la faraja sana kwa makocha kutoka Ulaya kuona nimekuwa mchezaji bora wa mechi. Ni hatua kubwa kwenye maisha yangu ya soka," alisema Kaseke.

Chanzo: mwananchi.co.tz