Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaseja amejitenga na ufalme wake

Kaseja Pic Data Kaseja amejitenga na ufalme wake

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

NYUMA ya pazia, imefahamika uwezo anaouonyesha kipa wa KMC, Juma Kaseja kwa asilimia kubwa unabebwa na nidhamu, uchu wa mafanikio, kuheshimu miiko ya soka na bidii.

Jina lake linazidi kukua tangu lianze kusikika kwa wadau wa soka hata baada ya kuzichezea Simba na Yanga kwa mafanikio na sasa akiwa KMC.

Jambo hilo limewaibua wadau na makocha wa soka kumzungumzia Kaseja na Kocha wa makipa, Idd Pazi alisema nyota huyo amekuwa akifanya mazoezi ya ziada tofauti na makipa wa sasa ambao ni kama wameridhika na mafanikio kidogo wanayoyapata na kisha wanapotea kwenye ramani.

“Kaseja haishii kwenye mazoezi ya kocha tu, nakumbuka mwaka 2009, nikiifundisha Moro United, kambi tuliweka Kijitonyama, Simba ilikuwa haifanyi mazoezi asubuhi, hivyo alikuwa anakuja na mipira yake kwenye gari,” alisema Pazi na kuongeza;

“Nilikuwa nikimaliza mazoezi na timu yangu, namfundisha Kaseja kwa dakika 50 na jioni alikuwa anakwenda kujiunga na timu yake. Hili liliwahi kuniletea shida kwa kiongozi mmoja aliyekuwa kwenye kamati za Yanga. Hata hivyo, nilimwambia siwezi kuacha kuendeleza kipaji cha kijana wangu kisa utani wao wa jadi.” Kuhusu kipa Ivo Mapunda, Pazi alisema; “Mapunda alikuwa anaelekea mwisho. Naye alikuwa anapenda sana mazoezi. Kuhusu taulo lake alikuwa anawachanganya tu. Hivyo, bado sijaona makipa wanaofikia levo zao wakati huu.”

Akiunga mkono hoja ya Pazi, straika wa zamani wa Simba, Idd Pazi Samatta alisema; “Kaseja anabebwa na kujiamini, mazoezi magumu yanayomweka fiti na anaifikiria zaidi kesho yake na siyo kujibweteka na mafanikio yake.

“Kwanza mwonekano wake unaonyesha ni mtu wa mazoezi makali, nani asiyejua umaarufu wa Kaseja, ingekuwa mwingine basi angevimba kichwa na kuona amemaliza, naona amejiongeza na kwenda kusomea ukocha, kifupi anajitambua.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz