Rais wa TFF, Wallace Karia amesema ana mkakati wa kuanzisha tuzo ya mwenyekiti bora wa Chama cha mkoa (FA).
Katiba hotuba yake ya nusu saa kablw ya kufunga mkutano wa TFF baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu mjini Tanga, Karia amesema mshindi wa tuzo hiyo atapata Sh10 milioni kwenye mkoa wake.
"Lengo ni kuwa na vyama vya mikoa imara, tukifanikiwa huko zawadi ya Sh 10 milioni itaelekezwa kwenye maendeleo ya soka la vijana.
Amesema pia ana mkakati wa kuanzishwa Ligi ya vijana chini ya miaka 17 ya klabu kila mwaka.
"Itachezwa kwenye mikoa, kanda na kisha taifa," amesema.
Pia amevitaka vyama shiriki vya makocha, wachezaji, waamuzi na soka la wanawake kufanya kazi kwa bidii ili kuboresha sekta hizo.