Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karia ataka ushindani zaidi Ligi Kuu

9859 Kiria+pic TZWeb

Sun, 24 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amezitaka timu za Ligi Kuu kutumia vyema fursa ya ongezeko la idadi ya timu za ligi msimu ujao kuleta maendeleo ya soka nchini.

Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo za Ligi Kuu 2017/2018 Rais Karia alisema ongezeko la timu ni nafasi ya kipekee ya soka la Tanzania kupiga hatua iwapo klabu zitaleta ushindani wa kweli.

"Niwapongeze kamati ya tuzo kwa kazi nzuri waliyoifanya. Kama ambavyo imeshasemwa awali kuwa lengo la tuzo hizi ni kuongeza ushindani wa ligi.

Hivyo tunaamini tuzo hizi zinazotolewa leo zitakuwa chachu ya kuongeza hamasa na ushindani kwenye ligi jambo ambalo litasaidia kukuza soka letu," alisema Karia

Chanzo: mwananchi.co.tz