Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karia aendelea kuandamwa kwa kauli yake dhidi ya Tundu Lissu

39855 Pic+karia Karia aendelea kuandamwa kwa kauli yake dhidi ya Tundu Lissu

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baadhi ya wananchi na wanasiasa wameendelea kumshukia Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kutokana na kauli yake aliyoitoa jana Jumamosi dhidi ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.

Jana akiwa katika mkutano mkuu wa TFF jijini Arusha, Karia alikemea watu wenye tabia za ‘u Tundu Lissu’ katika soka, kwamba hawezi kukubali kuona wakiendelea kuukosoa uongozi wa shirikisho hilo.

Katika mkutano huo, alimfananisha aliyekuwa makamu wa rais wa TFF, Michael Wambura na Lissu kwa kupinga hoja, hatua ambayo iliwaibua Chadema na kumtaka Karia kuomba radhi kutokana na kitendo hicho.

Wanasiasa na wananchi hao, wamemshukia Karia kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii na ile ya Facebook ya Mwananchi baada ya habari hiyo kuwekwa kwenye mtandao.

Akichangia katika akaunti ya Facebook ya Mwananchi, Didas Tumaini amesema kitendo cha aibu alichokifanya Karia cha kuliingiza soka la Tanzania kwenye siasa. “Amwache tu huyu binadamu anayeitwa Lissu, ameshindikana kwenye risasi sidhani kama kwenye soka atatufaa. Nadhani ungejaribu kutafuta mbinu za kuboresha soka la Tanzania kuliko kuanza kutafuta ligi na Lissu. Huyu jamaa kwake jela ni kama saluni, anaingia na kutoka.”

“Tumwache Lissu labda ni mpango wa Mungu kwa Watanzania, sisi tukae chini tujiulize kwa nini tunashindwa hadi leo. Lissu kama mganga wa kienyeji haishiwi nyimbo. Sisi tujadili tu kwa nini tulishindwa kuwafunga Lesotho, tujadili je kama tutamfunga Mganda,” anasema Tumaini. Tumaini anasema ni vyema Karia angetafuta mbinu mbadala kuhakikisha soka Tanzania angalau linafikia viwango vya nchi jirani ya Kenya, huku akimuuliza haumizwi na kitendo cha timu ya Taifa kushikwa sharubu kwenye uwanjani wa nyumbani. 

Katika akaunti yake ya Twitter Meya wa Ubungo Boniface Jacob? @MayorUbungo ameandika, “Watanzania tunapenda sana mpira, kinachotugharimu ni kuacha vyama vya mpira wa miguu kama @Tanfootball kuongozwa na wababaishaji na matapeli, tusitegemee maajabu katika soka kuanzia vilabu vyetu hadi timu ya Taifa.”

Naye Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema),Godbless Lema? ameandika, “michezo ina nafasi kubwa ya kuunganisha makabila, mataifa duniani, kutumia jukwaa la michezo kugawa watu ni hatari kwa michezo usalama. Chadema itachukua hatua FIFA dhidi ya Wallace Karia.”

Hata hivyo baadaye Karia aliomba radhi kwa kauli hiyo pale aliposema: “Kama kauli hii imewakera wengine naomba samahani.”



Chanzo: mwananchi.co.tz