Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karia: Tungefuata matakwa ya wadhamini, TFF ingedharaulika

39732 PIC+WADHAMINI Karia: Tungefuata matakwa ya wadhamini, TFF ingedharaulika

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha.Wakati kukiwa na sintofahamu ya udhamini kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Rais wa Shirikisho, Wallace Karia amesema ilikuwa lazima wapinge matakwa ya wadhamini wao kwa maslahi ya Shirikisho. Katika hotuba yake kwenye mkutano mkuu wa TFF unaoendelea mjini hapa, Karia alisema matakwa ya wadhamini wao hayakuwa na tija kwenye Shirikisho. "Hata kama ni maskini, sio kila kitu ukubali, kama Leo hii TFF tungefuata matakwa ya wadhamini wetu, basi Leo hii tungeonekana kichekesho," alisema. Bosi hiyo wa mpira nchi alisema hakuna mdhamini aliyesitisha mkataba na TFF. "Wadhamini wetu wote wapo, Hata Vodacom hawajaondoka, tulishindwana kwenye matakwa, lakini sasa mazungumzo yanakwenda vizuri," alisema Karia.

Chanzo: mwananchi.co.tz