Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kapombe aumia mazoezini hatihati kuikosa Afcon

61092 Pic+kapombe

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Beki wa kulia wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Shomari Kapombe hatakuwa katika kikosi kitakachoenda Misri.

Kapombe aliitwa katika kikosi cha Taifa Stars huku akiwa bado majeruhi aliyoyapata katika kambi ya timu hiyo Afrika Kusini wakijiandaa kucheza na Lesotho.

Wachezaji wa Taifa Stars walilipoti kambini Juni 2, Kapombe akiwa miongoni mwao, lakini alikuwa akifanya mazoezi maalumu chini ya uangalizi wa madaktari.

Taarifa ambazo Mwanaspoti imezipata kuwa Kapombe wakati akiendelea na mazoezi hayo alijitonisha jambo ambalo limemfanya kuondoka kambini.

Kapombe hataweza kuwa katika kikosi cha Taifa Stars kinachoendelea na mazoezi kila siku asubuhi na jioni katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, na hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachokwenda Misri.

Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Clifford Mario Ndimbo alisema mazoezi maalumu anayofanya Kapombe anashirikiana na madaktari wa Simba na Taifa Stars.

Pia Soma

Ndimbo alisema siku ya mwisho ya kambi hapa Dar es Salaam, ndio kocha ataamua kuwa Kapombe atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoondoka au hatakwenda.

"Madaktari wanaendelea na ratiba yake Kapombe ili kuona kama anaweza kwenda kwenye mashindano, lakini tofauti na hivyo tutaekeza pia," alisema Ndimbo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz